Akamatwa na heroin Tanga

0
141

Hamad Mbaraka mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa barabara ya 19 eneo la Ngamiani Kusini mkoani Tanga, amekamatwa akiwa na gramu 500 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Tanga Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini James Kaji amesema kuwa, Hamad amekamatwa kufuatia ushirikiano baina ya Wananchi na vyombo vya Ulinzi.