Akamatwa kwa kumpiga mpeziwe risasi wakiwa hotelini

0
377

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Salum Othuman (44) kwa tuhuma za kuwajeruhi watu watatu akiwemo mpenzi wake, Happiness Israel (32).

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amebainisha kuwa mtuhumiwa ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya dhahabu jijini Mwanza alimpiga mpenzi wake risasi ya mguuni baada ya kuibuka ugomvi kati yao wakiwa chumbani hotelini.

Baada ya kutenda kosa hilo alimbeba Happiness kwa lengo la kutaka kuondoka nae, ndipo meneja wa hoteli alipomuona na kumzia.

Kamanda huyo amesema meneja huyo alilazimika kumpisha mfanyabiashara huyo baada ya kutishia kutaka kumpiga risasi, na alipoingia kwenye gari alimgonga meneja huyo na kumsababishia majeraha mbalimbali.

Meneja wa hoteli na Happiness wote wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita na Hospitali ya Rufaa ya Bugando, mtawalia.