Waziri Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa idhini ya ajira za watumishi wa Sekta ya Elimu na Afya 17,412 ambapo nafasi 9,800 ni za walimu na 7,612 ni za kada za afya ambao wataajiriwa katika mwaka huu wa fedha 2021/22.
Bashungwa ametoa taarifa rasmi kuwa Watanzania wenye sifa wanaelekezwa kuanza kuomba kuanzia leo. Aidha, amewaelekeza kuwa maombi ya ajira hizo ni bure na yanafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki ambao maelekezo yake yatakuwa katika tangazo la ajira.
Asilimia tatu (3%) ya ajira hizo ni za Watu wenye Ulemavu kulingana na Sheria.
Pia ameelekeza wakurugenzi wote wa hamashauri kuhakikisha wanawanunulia watu wenye ulemavu wa ngozi mafuta kwa ajili ya kulinda ngozi zao.