Ajifungua watoto tisa kwa uzao mmoja

0
219

Halima Cisse, raia wa Mali mwenye umri wa miaka 25 amejifungua watoto tisa kwa uzao mmoja (nonuplets)
kwa njia ya upasuaji.

Upasuaji huo umefanyika nchini Morocco, lakini kabla ya kupelekwa nchini humo Halima alilazwa katika hospitali moja iliyopo katika mji mkuu wa Mali – Bamako kwa muda wa wiki mbili.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, Mwanamke huyo pamoja na watoto wake tisa – wa kike watano na wa kiume wanne wanaendelea vizuri.

Halima Cisse ameweka rekodi ya kujifungua watoto wengi kwa uzao mmoja baada ya Nadya Suleman, ambaye mwaka 2009 alijifungua watoto nane – wa kiume sita na wa kike wawili huko California nchini Marekani na kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia
(Guinness World Record).

Kwa sasa rekodi hiyo inashikiliwa na Halima Cisse.