Ajali yaua watumishi wa TANESCO

0
184

Watumishi watatu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) mkoa wa Manyara, wamefariki dunia katika ajali iliyotokea kwenye barabara ya Babati Singida.

Habari zaidi kutoka mkoani Manyara zinaeleza kuwa, watumishi hao wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakitumia aina ya
Toyota Land Cruiser kugongwa na roli linalodaiwa kupata hitilafu katika mfumo wake wa breki.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya TANESCO mkoa wa Manyara imewataja watumishi waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Loren Materu, Emmanuel Thobias na Nassoro Mtime.

Majeruhi wengine watatu katika ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Mrara, kwa ajili ya kupatiwa matibabu.