Ajali yaua wanne Bagamoyo

0
169

Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Prado
kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la Mapatano wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda ya Polisi wa mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia hii leo na
na kuongeza kuwa watu wote waliofariki dunia walikuwa ndani ya Prado.

Amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Nech Msuya ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya APSA, Dayana Mageta, Norah Msuya – Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe na abiria mwingine wa kike ambaye bado hajatambuliwa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na lori hilo la mizigo.

Miili yote ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika zahanati ya Lugoba mkoani Pwani.