Ajali yaua 12 Dodoma

0
846

Watu 12 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 60 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester lililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar es Salaam, ambalo limegongana uso kwa uso na lori lenye shehena ya saruji.

Ajali hiyo imetokea saa sita usiku kuamkia leo Februari 9, 2023 katika kijiji cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.