Ajali yagharimu maisha ya watumishi 5 TRA

0
782

Watumishi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamefariki dunia baada ya gari aina ya Landcluser walilokuwa wakitumia kugonga kwa nyuma Lori aina Fuso.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Taarifa za awali zinadai kuwa Watumishi hao walikuwa kazini, ambapo walikuwa wakitumia gari hiyo kufukuza gari nyingine iliyohisiwa kubeba bidhaa za magendo.