Ajali ya ndege yaua waziri na naibu wake

0
223

Watu 18 wakiwemo waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine wamefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea katika mji wa Brovary
karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Kyiv.

Watu tisa kati ya waliofariki dunia walikuwa ndani ya helikopta.

Habari zaidi kutoka nchini Ukraine zinaeleza kuwa watu wengine zaidi ya 20 wanaendelea kupatiwa matibabu baada ya kupata majeraha kufuatia ajali hiyo.

Helkopta hiyo imeanguka katika eneo la makazi ya watu ambapo ni karibu na shule ya awali