Ajali ya ndege, Rais Samia atuma salamu za pole

0
428

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision Air PW 494, iliyokuwa inatoka mkoani Dar es Salaam kuelekea Bukoba Mkoani Kagera kupitia mkoani Mwanza imeanguka katika Ziwa Victoria mapema asubuhi ya leo

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera, William Mwampagale, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya ndege ya Precision Air majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kubainisha kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa kutokana na mvua zinazonyesha mkoani humo

Kutokana na taarifa za ajali hiyo Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia ukurasa wake wa twitter ametuma salamu za pole kwa wote walioathirika na ajali hiyo na kuwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati zoezi la uokoaji likiendelea

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), mapema limezungumza na Mwandishi wake wa habari mkoani Kagera, Charles Mwebeya akiwa katika eneo la tukio na kueleza kuwa zoezi la uokoaji linaendelea kupitia vikosi mbalimbali vya uokoaji huku wakipata msaada mkubwa kutoka kwa wavuvi na wananchi wa eneo hilo

Endelea kufuatilia vyanzo yetu vya habari na mitandao yetu ya kijamii kupata taarifa zaidi.