Ajali ya ndege ndogo yaua watu wawili Seronera

0
149

Watu Wawili wamekufa baada ya ndege ndogo ya abiria kuanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera huko Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza na TBC kwa njia ya simu, Msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), -Pascal Shelutete amesema kuwa, ndege hiyo mali ya kampuni ya Auric Air imeanguka asubuhi hii wakati ikitoka katika uwanja huo kuelekea eneo la Gruneti ikiwa na abiria mmoja na rubani.