Ajali ya gari yasababisha vifo vya askari Wawili

0
289

Askari Wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 24KJ mkoani Kigoma, wamefariki Dunia na wengine zaidi ya Kumi wamejeruhiwa, katika ajali ya gari iliyotokea kwenye hifadhi ya Katavi.

Askari hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi lililokuwa limebeba silaha kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni mkoani Katavi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kigoma -Maweni,- Lameck Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi pamoja na miili ya askari hao wawili.

Amewataja Askari waliofariki Dunia kuwa ni Bakari Juma Mohamed na Rashid Abed Mwimbe.