Ajali Geita yaua 7

0
158

Watu 7 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 10 wamejeruhiwa mkoani Geita, katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Sheraton.

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika kijiji cha Mwilima kata ya Kasamwa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi hilo ambapo dereva alishindwa kulimudu, na hivyo kuliingiza basi hilo darajani.

Basi hilo lilikuwa katika safarri zake za kawaida kutoka mkoani Mwanza kuelekea mji wa Ushirombo, uliopo halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita na majeruhi wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kasamwa kilichopo halmashauri ya mji Geita.