Ahukumiwa miaka Saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kumficha mtoto

0
201

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Njombe, imemuhukumu kifungo cha miaka Saba jela Joel Nziku, baada ya kupatikana na hatia ya kumficha mtoto Gaudence Kihombo.

Nziku pia anashitakiwa kwa kosa la mauaji ya watoto Watatu wa familia moja na ni miongoni mwa Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe, ambapo takribani watoto Kumi waliuawa.

Mauaji hayo yalianza mwezi Novemba mwaka 2018, ambapo baadhi ya watoto waliouawa walikutwa wamenyofolewa viungo mbalimbali.