Afrika yatakiwa kuwa moja kwenye masuala ya sayansi

0
70

Imeelezwa kuwa mtazamo hasi wa kuona bidhaa zinazovumbuliwa Afrika ni hafifu, ndio unaosababisha teknolojia mbalimbali kutotambulika ipasavyo kimataifa.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) Profesa Fredrick Kahimba katika mkutano wa kimataifa wa Sayansi unaoendelea nchini Afrika Kusini.

Amesema kumekuwepo na mashine nyingi ambazo ni imara na zinazoendana na mazingira ya kutatuta changamoto za Kiafrika, lakini hazikubaliki na kupewa kipaumbele kutokana na mtazamo hasi.

Aidha, Profesa Kahimba amesema ili teknolojia za Afrika zikubalike ni lazima nchi za bara hilo zikubali kushirikiana katika masuala ya sayansi kwenye vumbuzi za teknolojia na soko la teknolojia husika.

Pia amebainisha kuwa TEMDO imeweka nguvu kubwa katika kutafuta soko la teknolojia zake kwenye soko la ukanda wa Kusini yani SADC, ambapo mpaka Sasa wameuza teknolojia ya viwanda nchini Afrika Kusini na Ethopia.