Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Maji kwa nchi za Afrika umeanza leo Jijini Dar es salaam huku ajenda ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na uondoshwaji wa maji taka kwa nchi za Afrika.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano huo Waziri wa Maji wa Tanzania ambaye ndio Mwenyekiti wa Mkutano huo Profesa Makame Mbarawa amesema kutokana na umuhimu wa Maji kwa wananchi imekuwa ni utamaduni wa Mawaziri hao kukutana na huu ni Mkutano wa Tisa ukiwa umejikita katika kuhakikisha wanamaliza changamoto ya maji.