Afisa Usalama na Polisi feki waonja joto ya jiwe

0
401

Raia wawili wa Tanzania wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na Askari Polisi na kutumia vyeo hivyo kutapeli wananchi.

Patrick Tarimo (32) anashikiliwa kwa kumtapeli raia wa kigeni shilingi milioni 20 baada ya kumkamata na kujitambulisha kama afisa Usalama wa Taifa.

Mwengine ni Castory Wambura (57) anayeshitakiwa kwa kudhulumu shilingi milioni15 kutoka kwa wafanyabiashara watano wa Kariakoo baada ya kujitambulisha kama ofisa wa polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewaomba wananchi kuwafichua wahalifu katika maeneo mbalimbali ya nchi na pia kuwasiliana na polisi wanapokuwa na wasiwasi na watu wanaojitambulisha kwa cheo cha maofisa wa polisi.