Afariki Dunia baada ya kufukiwa na kifusi

0
173

[1:26 AM, 9/10/2019] Maria TBC Online: Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine Wanane wameokolewa, baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu ya Shilalo yaliyopo kwenye kata ya Inonelwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, – Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa vikosi vya uokoaji vinamtafuta mtu mwingine ambaye anadhaniwa bado amenasa katika kifusi hicho.

Kamanda Muliro amesema kuwa, tukio hilo limetokea saa Saba usiku wa kuamkia hii leo, ambapo watu hao Kumi waliingia katika machimbo hayo kwa ajili ya kufanya kazi zao za uchimbaji kama kawaida.

Amesema kuwa, mara baada ya kuingia kwenye machimbo hayo, kifusi kiliporomoka na kuwafukia ambapo jitihada za uokoaji zilianza mara baada ya tukio hilo.
[1:26 AM, 9/10/2019] Judith ene Laizer: leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia kujiua inayoadhimishwa kila mwaka Septemba 10.Idadi ya nchi zenye mikakati ya kitaifa ya kuzuia watu kujiua imeongezeka katika kipindi cha miaka mitano tangu shirika la afya duniani WHO lilipotoa ripoti ya kwanza ya dunia kuhusu matukio hayo.