Abbas Mtemvu Mwenyekiti mpya CCM Dar

0
87

Abbas Mtemvu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam.

Mtemvu amepata kura 444 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Kate Kamba ambaye alikuwa akitetea kiti hicho.

Wengine walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho ni Baraka Konisaga aliyepata kura nne na Jamal Rwambow aliyepata kura mbili.

Uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam umesimamiwa na Fatma Mwasa ambaye ni mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Abbas Mtemvu amewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Temeke mkoa wa Dar es Salaam.