Serikali kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya Maendeleo

0
177

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua miradi ya maendeleo, kituo cha polisi Kizimkazi, ofisi ya Sheha na ofisi ya CCM Tawi la CCM Miwaleni zilizopo wilaya ya kusini katika Mkoa wa Kusini Unguja leo katika ziara yake visiwani Zanzibar

Akizindua jengo la Ofisi ya Sheha Tasani iliyopo Makunduchi wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja, Rais Samia amesema serikali itaendelea kuimarisha na kujenga miradi ya Maendeleo vituo vya afya na elimu ili kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika eneo hilo

Katika ziara yake Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Kilele cha Siku ya Kizimkazi inayotarajia kufanyika kesho tarehe 3 Septemba katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani