21 wasimamishwa kazi tukio la kuungua ghala

0
81

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amewasimamisha kazi watumishi 21 mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na hujuma katika tukio la moto lililochoma ghala la kuhifadhi bidhaa za magendo kwenye bandari ya Tanga mwezi Oktoba mwaka huu.

Mgumba amefikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi kuhusu tukio hilo kutoka kwa kamati ya kuchunguza tukio hilo aliyoiunda Ili kuchunguza chanzo cha moto huo.

Amesema watumishi hao wamesimamishwa kazi Ili kupisha uchunguzi kutokana na kuitia hasara serikali baada ya tukio hilo la kuungua moto
ghala la kuhifadhia bidhaa za magendo kwenye bandari ya Tanga.