10 wahukumiwa kunyongwa Tanga

0
150

Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu kifungo cha maisha na kunyongwa hadi kufa washtakiwa 10 kwa kosa la mauaji ya Mbwana Salim Kilo aliyekuwa mlinzi wa ofisi ya kijiji cha Lulago wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Washtakiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 10, 2013 katika kijiji cha Lulago Kilichopo wilaya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi Kanda ya Tanga, Latipha Mansoor amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili, Mahakama imejiridhisha na kuwatia hatiani.

Waliohukumiwa ni Haji Omary Mzana, Khalid Salehe Sekinzu, Omary Said, Toba Salehe Sekinzu, Abdallah Mrisho, Mnyamisi Said, Abdulrahman Hassan, Juma Omary, Ramadhani Athuman Mnguu na Jawa Omari Mzana.

Awali washtakiwa hao walikua 20 ambapo walishtakiwa kwa kosa la ugaidi huku tisa kati yao wakiachiwa huru mwaka 2022 baada ya Mahakama kukosa ushahidi na baadae mashtaka yakabadilishwa na kuwa kesi ya mauaji namba 22 ya mwaka 2022.

Leo ambayo ni siku ya kutolewa kwa Hukumu, mshtakiwa mmoja ameachiwa huru baada ya upande wa ushahidi kuonyesha kuwa ameshtakiwa kwa jina lisilokuwa la kwake.

Katika kesi hiyo upande wa washtakiwa ulikua na mashahidi tisa wakati upande wa utetetzi walikua 20.