​Madiwani Temeke walia na watendaji

Temeke Dar es salaam

0
147

Baraza la madiwani la Manispaa ya Temeke limeagiza watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa taarifa za mipango miji katika kata ili kuondoa mkanganyiko unaotokea baina ya madiwani na wananchi kuhusu uwekezaji wa ardhi.

Wakichangia taarifa zilizowasilishwa katika Baraza hilo na watendaji wa halmashaauri hiyo, Baadhi ya madiwani wamesema kwa sasa idara ya mipango miji imekuwa ikigawa maeneo bila kuwashirikisha madiwani.

​Madiwani hao wamemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anatoa taarifa za ugawaji wa maeneo katika kata zao ili kupunguza migogoro inayojitokeza kati ya madiwani na wananchi ​

Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa hiyo Arnold Peter amesema maelekezo yaliyotolewa kwenye Baraza hilo lazima yatekelezwe ili kuondoa sintofahamu baina ya madiwani na wawekezaji katika maeneo yao huku kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Else Kimaro akiahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa katika Baraza hilo.

Kikao hicho cha robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha kimepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi katika kata zote za Manispaa hiyo.​