Zimbabwe hii leo imeanza rasmi maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha
Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe, aliyeliongoza Taifa hilo kwa miaka 37.
Baadhi ya Raia wa Zimbabwe wametoa maoni yao na kueleza kuwa, Mzee Mugabe alitumia nguvu zake zote kulipigania Taifa hilo.
Nacho chama cha ZANU-PF kimemtangaza Mugabe kuwa ni shujaa wa Taifa hilo na kwamba ataendelea kuenziwa na vizazi vyote nchini Zimbabwe.
Mzee Mugabe aliyekuwa na umri wa miaka 95, alifariki dunia hapo jana
nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi Aprili mwaka huu.
Hadi sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu mazishi ya Kiongozi huyo, lakini Serikali ya Zimbabwe kupitia Ubalozi wake nchini singapore
imesema kuwa, taratibu zinazoendelea hivi sasa ni kuusafirisha mwili wa kiongozi huyo na kuurudisha nchini mwake.