Kiongozi wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema ameshinda kiti cha Urais.
Hichilema amepata kura 2,810,757 dhidi ya Rais anayemaliza muda wake, Edgar Lungu ambaye amepata kura 1,814,201.
Hichilema ambaye ni kiongozi wa chama cha UPND anakuwa Rais wa awamu ya saba kuitumikia Jamhuri ya Zambia.
Hata hivyo, Rais Lungu ameonesha kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi akidai kuwa ulighubikwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu.
Endapo Rais Lungu au mgombea mwingine hatoridhia matokeo hayo anatakiwa kufungua kesi ya kupinga matokeo katika Mahakama ya Katiba ndani ya siku saba tangu kutangazwa kwa matokeo.