Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limedai kuwa, zaidi ya watu Mia Moja wameuawa nchini Iraq tangu Ijumaa iliyopita, wakati wa maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya petroli.
Wakati Amnesty International ikitoa madai hayo, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Maafisa wa Usalama nchini Iraq, kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya Waandamanaji.
Katika siku za hivi karibuni, Raia wa Iraq wamekua wakiandamana kupinga masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na kupanda kwa bei za bidhaa.
