Yanga yatakata Tunisia

0
159

Mabingwa wa Tanzania Yanga wamethibitisha ubora wao ugenini nchini Tunisia baada ya kuiondoa Club Africain kwa bao moja kwa bila.

Bao la ushindi la Yanga katika mchezo huo limefungwa na nyota wake raia wa Burkina Faso Stephane Aziz Ki katika dakika ya 78 baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Fiston Mayele.

Yanga waliocheza kwa ustadi mkubwa wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu huu baada ya kuondolewa na Al Hilal ya Sudan katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.