Wimbo wa Taifa kupigwa akiwepo Rais tu – Sudan Kusini

0
326

Rais SALVA KIIR wa Sudan Kusini, amepiga marufuku kuimbwa kwa wimbo wa TAIFA wa nchi hiyo, katika halfa yoyote ambayo Rais huyo hajahudhuria.

Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa marufuku hiyo imetangazwa na waziri wa habari wa Sudan Kusini MICHAEL MAKUEI ambapo amesema wimbo huo wa taifa ni alama ya taifa hilo na utapigwa katika hafla itakayohudhuriwa na rais na si vinginevyo.

Waziri huyo amesema kumekuwa na baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali nchini humo ambao wamekuwa wakipiga wimbo wa taifa katika halfa mbalimbali jambo alilosema ni matumizi mabaya ya alama hiyo ya taifa la Sudan Kusini.

Hatua ya marufuku hiyo inaripotiwa kupitishwa na kikao cha baraza la mawaziri wa Sudan Kusini kilichofanyika mwishoni wa juma lililopita.