WHO yaitisha mkutano kujadili corona

0
443

Wawakilishi kutoka nchi 194 wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wameanza mkutano wao huo Geneva – Uswisi kwa lengo la kutathimini hali ya maambukizi ya virusi vya corona katika nchi mbalimbali duniani pamoja na kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo.

Mkutano huo ambao ni wa 73 wa WHO, unafanyika kwa njia ya mtandao ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Rais Xi Jing Ping wa China ameahidi serikali yake kutoa dola bilioni mbili za Kimarekani kwa Shirika hilo la Afya Duniani ili liweze kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona katika nchi mbalimbali duniani.

Rais Xi Jing Ping ameendelea kutetea hatua ambazo nchi yake imechukua kukabiliana na corona iliyoanzia nchini China na kusema kuwa itaendelea kutoa taarifa muhimu zitakazosaidia kupatikana kwa ufumbuzi na chanjo ya ugonjwa huo.