Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amemfukuza kazi Waziri wa Nishati wa nchi hiyo Joram Gumbo kufuatia nchi hiyo kuendelea kukumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, tatizo lililoanza mwaka 2016.
Rais Mnangagwa amefikia uamuzi huo kufuatia kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa raia wa nchi hiyo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, ambapo habari zaidi kutoka nchini humo zinasema kuwa umeme umekua ukikatika kati ya saa Tano na Nane kwa siku.
Sababu kubwa ya tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini Zimbabwe ni kushuka kwa uzalishaji katika chanzo kikuu cha uzalishaji na uchakavu wa mitambo ya uzalishaji kwa kutumia umeme wa Makaa ya Mawe.