Waziri wa Fedha wa Kenya amefikishwa mahakamani

0
224

Waziri wa Fedha wa Kenya, – Henry Rotich  amefikishwa mahakamani jijini Nairobi,  akituhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya, – Noordin Haji amesema kuwa Rotich pamoja na maafisa wengine wa serikali, wanatuhumiwa kukiuka taratibu za utoaji wa Kandarasi  ya zaidi ya Dola Milioni 450 za Kimarekani  iliyopewa kampuni ya Cmc Di Ravenna ya nchini Italia, kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa mawili ya maji.

Habari zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, mabwawa hayo mawili ya maji yalidaiwa kujengwa katika jimbo la Elgeyo Marakwet, lakini mpaka sasa fedha za ujenzi wa mabwawa hayo hazijulikani zilipo na mabwawa hayo hayajajengwa.

Hapo jana, Rotich  alijisalimisha kwa Maafisa wa upelelezi, muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya kuagiza akamatwe.

Kampuni hiyo ya Cmc Di Ravenna pamoja na Waziri Rotich  wamekanusha tuhuma hizo.