Waziri Mkuu wa Uingereza akutwa na virusi vya corona

0
697

Waziri Mkuu wa Uingereza amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID-19).

Boris Johnson ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali katika mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Hadi sasa nchi hiyo imethibitisha kuwapo kwa visa 11,658 vya waathirika, ambapo vifo ni 578, huku waliopona wakiwa 135.