Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni siku 45 tu tangu ashike wadhifa huo.
Truss ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari na anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Uingereza kuhudumu katika kipindi kifupi.
Pamoja na kutangaza uamuzi huo, Liz Truss ataendelea kuongoza kama Waziri Mkuu wa Uingereza hadi mrithi wake atakapochaguliwa.