Waziri Mkuu wa Ivory Coast afariki dunia

0
367

Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Gon Coulibaly amefariki dunia muda mfupi baada ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri katika ofisi ya Rais mjini Abidjan.

Amadou alikuwa akitarajiwa kuwa mrithi wa Rais wa sasa wa Ivory Coast,
Alassane Ouattara katika uchaguzi wa Rais unaotarajiwa kufanyika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Habari zaidi kutoka nchini Ivory Coast zinaeleza kuwa kwa muda wa miezi miwili Amadou mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo na kwamba alianguka chini ghafla na kupoteza fahamu na kukutwa na umauti.