Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi, amelaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ndani ya ardhi ya nchi yake.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu huyo imesema mashambulizi hayo ya Marekani dhidi ya jeshi la Iraq hayakubaliki, na yana matokeo ya hatari.
Maelfu ya raia mjini Baghdad hii leo wameonekana wakiandamana katika balozi za marekani kupinga hatua hiyo ya mashambulizi.
Jumapili, jeshi la Marekani liliwashambulia wanamgambo wa kundi la Kataib Hizbullah, kulipiza kisasi mauaji ya mkandarasi mmoja wa Kimarekani kwenye kambi ya kijeshi ya Iraq ambapo Wapiganaji 25 waliuawa na wengine 55 kujeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.