Watumishi wa Umma KENYA kuvaa mavazi ya asili

0
781

Serikali ya Kenya imewaagiza Watumishi wote wa Umma nchini humo kuvaa mavazi ya asili yanayolitambulisha Taifa hilo pamoja na yale yaliyotengenezwa nchini humo kwa siku za Ijumaa na Sikukuu.

Agizo hilo limesainiwa na Wakili Mkuu wa Kenya, – Kennedy Ogeto na kuchapishwa katika gazeti la Serikali.

Habari kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, agizo hilo lina lengo la kuviimarisha viwanda vya ndani, soko la ndani na kuongeza ajira, mambo ambayo yamekua yakikisisitizwa mara kwa mara na Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo haijafahamika kama kutakua na adhabu yoyote itakayotolewa kwa Watumishi wa Umma ambao watashindwa kutii agizo hilo la kuvaa mavazi ya asili yanayolitambulisha Taifa la Kenya pamoja na yale yaliyotengenezwa nchini humo kwa siku za Ijumaa na Sikukuu.

Wakati wa sherehe za siku ya Mashujaa zilizofanyika hivi karibuni huko Mombasa nchini Kenya, Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto walionesha mfano kwa kuvaa mavazi yaliyotengenezwa nchini humo, huku Mawaziri, Naibu Mawaziri na Viongozi wengine wa Serikali nao wakiwaunga mkono.