Watu sita wamekufa Mashariki mwa Afghanistan, baada ya kutokea shambulio la kigaidi lililokuwa limewalenga Raia wa kigeni.
Miongoni mwa watu waliokufa katika tukio hilo ni daktari mmoja raia wa Japan, aliyekuwa akitoa misaada ya kibinadamu nchini humo.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Jalalabad, baada ya watu wenye silaha kushambulia Raia hao wa kigeni, na daktari huyo Raia wa Japan ndiye aliyekuwa Mkuu wa Shirika la nchi hiyo lililokuwa likitoa misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan.
Habari zinasema mara baada ya wahusika kushambulia gari la wageni hao walikimbia, na kutokomea kusikojulikana.