Watetezi wa haki za binadamu Afrika wampongeza Rais Samia

0
150

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kuendelea kufanya kazi na watetezi wa haki za binadamu nchini na kwamba ni jambo linalofanya haki za binadamu kufuatwa nchini humo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Afrika (Pan-African Human Rights Defenders) Hassan shire leo tarehe 15/6/2022 katika kikao cha 50 cha Baraza la Haki za Binadamu duniani kinachoendelea Geneva Uswisi.

Shire amewaomba viongozi wengine Duniani kuiga mfano huo wa Rais Samia wa kuzingatia haki za binadamu.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania mjini Geneva Balozi Hoyce Temu.