Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahamoud Thabit Kombo ametoa wito kwa watanzania wanaoishi nchini humo kujiunga na Jumuiya ya watanzania wanaoishi Italia, ili iwe rahisi kusaidiwa pindi wanapopata matatizo.
Balozi Mahamoud Kombo ametoa kauli hiyo nchini Italia aliposhiriki sala na dua ya kumuaga marehemu Mustafa Munawar, mtanzania aliyekuwa akiishi nchini humo.
Balozi huyo wa Tanzania nchini Italia ametoa kauli hiyo kufuatia changamoto zilizojitokeza katika kupata vibali vya kusafirisha mwili wa Munawar, ambaye hakuwa amesajiliwa katika Jumuiya ya watanzania wanaoishi Italia.