Watano wahukumiwa mauaji ya Khashoggy

0
412

Marekani imesema kuhukumiwa kwa watu watano wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi,ni hatua muhimu huku  baadhi ya maafisa wa Umoja wa Mataifa na nchi ya uturuki wamekosoa hukumu hiyo na kusema wale wahusika wakuu ambao washirika wa mwanamfalme Mohamed Bin Salman hawajawajibishwa.

Habari zinaeleza kuwa mahusiano ya karibu baina ya marekani na Saudi Arabia,yamekuwa yakikosolewa ikiwemo hatua ya Rais Donald Trump kukataa kura ya bunge la Congress iliyoamua kwamba Marekani isitishe uungaji mkono wake kwa Saudi Arabia katika vita vya Yemen.