Watakaoandamana Sudan Kusini kukabiliana na Dola

0
448

Ulinzi umemarishwa katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa Sudan Kusini, –  Juba huku ukaguzi mkali ukiendelea nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwatafuta vinara wa maandamano nchini humo.

Sababu kubwa ya kuimarishwa kwa ulinzi huo ni vikundi kadhaa kutangaza kufanyika kwa maandaano ya nchi nzima hii leo kushinikiza Rais Salva Kiir kuondoka madarakani na kutaka kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia.

Vikundi vilivyoandaa maandamano hayo vimesema kuwa wakati umefika kwa utawala wa Rais Kiir kuondolewa  madarakani pamoja na viongozi wote wanaomuunga mkono.

Katika taarifa yake Rais Salva Kiir amewaonya raia wote wa Sudan Kusini wanaotaka kuandamana kwa kusema kuwa watakabiliana na vikosi vya nchi hiyo, na kuyaita maandamano hayo kama jaribio la kutaka kuiangusha serikali yake.