Wanawake wanaharakati wafikishwa mahakamani Saudia

0
356

Kwa mara ya kwanza baada ya mwaka mmoja, Wanawake kadhaa wanaharakati raia wa Saudi Arabia waliokuwa wakishikiliwa nchini humo wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka.

Wanaharakati mbalimbali duniani wamekuwa wakiishinikiza serikali ya Saudi Arabia kuwaachia wanaharakati hao, baadhi yao wakiwa ni wanawake vijana kwa madai kuwa nchi hiyo imekuwa ikikiuka haki za binadamu.

Wanawake hao walishiriki katika maandamano ya amani ya kudai haki mbalimbali za wanawake nchini mwao, ikiwa ni pamoja na kupigania wanawake kupewa ridhaa ya kuendesha magari.