Makumi elfu ya watu wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Hayati Papa Benedict XVI huko Vatcan.
Mazishi ya kiongozi huyo mstaafu wa Kanisa Katoliki Dunia yanatarajiwa kufanyika Alhamisi ambapo yataongoza na Papa Francis, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuzikwa na mrithi wake.
Mapema leo asubuhi watu walianza kukusanyika kwenye viunga vya St. Peter’s Square tayari kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo aliyefariki Desemba 31, 2022 akiwa na umria wa miaka 95.
Mwili wake utawekwa katika jeneza la wazi kwa siku tatu katika Kanisa la Basilika la Mt. Petro mjini Roma ambalo ni kanisa kubwa kuliko yote duniani na hutumiwa sana na Papa.