Wananchi wa Sudan wameadhimisha mwaka mmoja tangu lilipoanza vuguvugu la maandamano ya kupinga Serikali, maandamano yaliyosababisha aliyekuwa Rais wa nchi Omar Al Bashir kuondoka madarakani.
Wakati wakifanya maadhimisho hayo, Wananchi hao wamesema kuwa bado hawajaona maana ya halisi ya mapinduzi waliyofanya ya kumuondoa Al Bashir madarakani, kwani mahitaji yao muhimu yaliyosababisha wao kushiriki katika maandamano ya kumkataa Mwanasiasa huyo bado hajatimizwa.
