Baadhi ya Wananchi wa Kenya wameanza kufanya juhudi binafasi za kuwatafuta ndugu zao ambao hadi sasa hawajulikani walipo, baada ya nchi hiyo hasa eneo la Pokot kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyokuwa yakiambatana na maporomoko ya udongo.
Watu hao hivi sasa wameamua kuchukua majembe na sululu kwenda katika maeneo ambayo wanadhani kuwa ndugu zao wanaweza wakawa bado wamefukiwa na matope na kuanza kufukua kwa matumaini ya kupata miili ya ndugu zao.
Baadhi wamefanikiwa kunasua miili ya ndugu zao, huku wengine wakiendelea na zoezi hilo.
Zaidi ya watu Sitini wamekufa nchini Kenya kutokana na mafuriko hayo yaliyokuwa yakiambatana na maporomoko ya udongo.
Mafuriko hayo yalisababisha uharibufu mkubwa wa mali pamoja na miundombinu, huku zoezi la uokoaji likikwamishwa na kuharibiwa kwa miundombinu.