Maelfu ya watu wamekusanyika mjini Minsk nchini Belarus kushiriki katika maandamano ya kuunga mkono serikali ya nchi hiyo, baada ya mfululilizo wa maandamano ya kupinga serikali yaliyokuwa yakiambatana na ghasia.
Waandamanaji wanaopinga serikali ya Rais Alexander Lukashenko wamekuwa wakimshinikiza mwanasiasa huyo kuachia madaraka kwa madai kuwa hakupata ushindi halali katika uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumapili iliyopita.
Lukashenko aliyepata ushindi wa kishindo ameendelea kusisitiza kuwa yeye ndiye kiongozi wa taifa hilo kwani amepata kura nyingi.
Baadhi ya viongozi wa serikali yake wameanza kuwaunga mkono waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi na kusema kuwa hawako radhi kushuhudia vitendo vya unyanyasaji wanaofanyiwa waandamanaji wanaopinga serikali ya nchi hiyo.