Wanamgambo wafanya mashambulio na kuua Niger

0
165

Vikundi vya Wanamgambo nchini Niger vimeshambulia vijiji vya Tchombangou na Zaroumdareye na kuua wakazi wengi wa vijiji hivyo.

Vijiji yalipotokea mashambulio hayo vipo katika eneo la mpaka wa nchi ya Niger na Mali pamoja na Burkina Faso, eneo ambalo limekuwa na mashambulio kama hayo mara kwa mara katika siku za hivi karibuni. Habari kutoka Niger zinaeleza kuwa, watu 49 wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa katika kijiji cha Tchombangou na katika kijiji Zaroumdareye wameuawa watu 30. Vikundi vya Wanamgambo vilivyofanya mashambulio hayo vinadaiwa kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al – Qaeda.