Wanamapinduzi wa Uturuki wamehukumiwa Kifungo cha Maisha Jela

0
239

Viongozi 141 wa mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa dhidi ya serikali ya rais Reccep Tayyip Ordegan wa Uturuki wamehukumiwa kifungo cha maisha jela, wengi wao wakiwa ni waliokuwa askari wa jeshi la nchi hiyo.

Jaribio hilo la mapinduzi dhidi ya serikali ya rais Ordegan lilifanyika mwaka 2016, watekelezaji wake wengi wakiwa ni askari. Watu wengine kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na jaribio hilo lililoshindwa la mapinduzi ya serikali ya Uturuki wanasubiri hukumu zao.

Zaidi ya watu 250 waliuawa wakati wa jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi na wengine zaidi ya elfu moja kujeruhiwa.