Wanafunzi wengine 84 waliotekwa nyara waokolewa

0
203

Polisi nchini Nigeria wamethibitisha kuwaokoa Wanafunzi 84 waliotekwa nyara hapo jana na watu wenye silaha kwenye jimbo la Katsina

Wanafunzi hao walitekwa nyara wakiwa njiani kurejea nyumbani ambako ni kijiji cha Mahuta, na walikuwa wakitoka kuhudhuria sherehe za kidini.

Habari zaidi kitoka nchini Nigeria zinaeleza kuwa, Wanafunzi hao wameokolewa baada ya majibizano ya risasi kati ya watu hao wenye silaha na askari wa vikosi mbalimbali vya serikali waliokuwa wakishirikiana na Wanakijiji.

Hilo ni tukio la pili la utekaji nyara Wanafunzi kutokea ndani ya kipindi cha siku Nane katika jimbo hilo la Katsina.

Katika tukio la kwanza, Wanafunzi 344 wa kiume wa shule moja ya bweni walitekwa nyara na watu wenye silaha na kuachiwa huru ikiwa imepita takribani wiki moja.