Wanafunzi waanza kurejea shuleni Kenya

0
161

Wanafunzi nchini Kenya wameanza kurejea shuleni na kuanza masomo, baada ya Serikali ya nchi hiyo kutangaza kufunguliwa kwa shule zote zilizokuwa zimefungwa kwa kipindi cha miezi 10 iliyopita.

Kenya ililazimika kufunga shule na shughuli nyingine za kibiashara kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Hata hivyo baadhi ya Walimu nchini Kenya wanailalamikia hatua hiyo ya Serikali kufungua shule na kusema kuwa ni mapema mno, kwani hakuna vifaa ya kutosha kuweza kuwakinga wao pamoja na Wanafunzi dhidi ya maambukizi mapya.

Wanasema moja ya changamoto iliyopo sasa, ni kujitenga kutoka mtu mmoja hadi mwingine wakiwa shuleni, ili kuepuka maambukizi mapya.